Kisiwa cha wanawake
View on Open Library ↗

Kisiwa cha wanawake

by

36 min read
Rate this book:
147 pages 2019

About This Book

"Hiki ni kisiwa cha mapenzi kilichokuwa kinawazwa na kila mwanaume-aliyesikia tetesi za kuwepo kwake kikiwa na wanawake wazuri kuliko wote duniani. Ni kisiwa kigeni ambacho hata kwenye Ramani ya Dunia hakipo. Kiliibuka ghafla miaka ya hamsini, na kupata umaarufu mwaka 2013. Ndipo watu wakafahamu kuwa kuna kisiwa ambacho kimegundulika katika Bahari ya Hindi; Karibu na Nchi ya Tanzania. Sifa kubwa ya Kisiwa hicho, ni kuishi watu wa jinsia moja tu!. Nao ni Wanawake. Ila Kisiwa hicho, kinalindwa na Majini wa Baharini na hakuna kiumbe anayeweza kukatisha salama na kukifikia Kisiwa hicho. Nyumba na mavazi yao vilinakshiwa kwa dhahabu, Almasi, rubi na madini mengine ambayo hayapo kwenye ulimwengu wetu tunaoishi. Kwa kuwa kwao madini yapo kila mahali wala uhitaji kuchimba ili uyapate. Unaokota kama uokotavyo mawe barabarani. Uzuri wa wanawake ambao haujawahi kutokea toka dunia inaanza, Walibarikiwa viumbe hao waliotokea kama uvoga kwenye Kisiwa cha peke yao. Taarifa hizo ziliwafikia vijana wengi hasa mabaharia ambao walikua na ndoto za kutajirika katika kisiwa hicho kilichokuwa na kila aina ya madini. Mara kwa mara zilisikika taarifa za upoevu wa watu waliojaribu kwenda kujaribu bahati zao. Hata baadhi ya wavuvi waliokuwa wakivua kwenye maji ya kina kirefu baharini, walipotea pia. Matuko hayo yalizidi kila siju na kusababisha kuwa tishio kwa wavuvi wavuao samaki kwenye maji ya kina kirefu. Vijana watukutu, Hija, Amani, Said, Beka na Philipo, wanaamua, kujitosa kweda katika Kisiwa hicho kwa madhumuni ya kutafuta utajiri. Pili kujionea jinsi maisha ya wanawake hao wanavyoishi bila wanaume. Watafanikiwa kufika kwenye kisiwa hicho kilichojaa maajabu?"--Page 4 of cover

Buy This Book

As an Amazon Associate and Bookshop.org affiliate, BookOrb earns from qualifying purchases.

Write a Review

Sign in to write a review.