Mfalme Ana Pembe
View on Open Library ↗

Mfalme Ana Pembe

36 min read
Rate this book:
138 pages 2021

About This Book

"Fasihi si lazima iwe na majawabu ya masuali wajiulizayo watu, maana mwanafasihi naye pia ni sehemu ya watu hao hao wenye maswali na wasiojuwa utatuzi wake. Lakini fasihi ina wajibu wa kipekee wa kuyauliza maswali hayo kwa njia ya kisanii kwa niaba ya wanajamii, maana "fasihi ni kiyoo cha jamii". Inaposomwa au kulumbwa, fasihi inapaswa kusimama imara kama nguzo ya jamii na kuwa ujasiri wa kuyasema yote bila kubakisha kitu. Kwa mara nyengine tena, Mohammed anaipa nafasi jamii yake kuyauliza maswali yale wanayojiuliza kila siku kuhusu maisha yao - yawe ya kisiasa, kiuchumi, kitamaduni - kwenye ngazi za mtu mmoja, mahusiano ya wanandoa, jamii na hata taifa. Mfalme ana pembe ni muakisiko wa masuali yasongayo roho kwenye jamii anayoiakisi mshairi huyu bingwa wa Kiswahili. Kama hukusoma kwenye Andamo, Siwachi Kusema, Kalamu ya Mapinduzi, Machozi Yamenishiya na N'na Kwetu, basi ndani ya Mfalme ana pembe, mwanafasihi huyu anakudhihirishia kosa ulilolifanya hapo kabla, na anakuasa usilirejee."--Page [4] of cover.

Buy This Book

As an Amazon Associate and Bookshop.org affiliate, BookOrb earns from qualifying purchases.

Write a Review

Sign in to write a review.